Header Ads

Diamond "Nimefanya Kolabo na Young Killer Kuinua Muziki wa Nyumbani"



Stori inayotrend kwa sasa katika social networks ni kuhusu Diamond Platnumz ambaye ni kiongozi wa WCB kuzindua brand yake ya ‘manukato’ yaitwayo Chibu Perfume ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki wake.


Mbali na uzinduzi huo wa Chibu Perfume, leo April 24 2017 kupitia XXL ya Clouds FM staa huyo wa Marry You ametoa tathmini ya Bongo fleva akisema kuwa umekuwa na ushindani mkubwa akidai umewashinda hata Wanigeria kwa sasa.


Aidha, Diamond amegusia kuhusu kufanya collabo na rapa Young Killer akisema amefanya naye kazi kwa lengo la kunyanyua muziki wa nyumbani kwa sababu kufanya kazi tena na Wanaigeria hakuwashtui watu kama zamani:“Kitu ambacho watu hawakifahamu, ukifanya kazi na Wanigeria watu hawashtuki kabisa. Nimefanya collabo na Young Killer kunyanyua muziki. Muziki wetu umekuwa wa kiushindani kabisa, lazima tujitume. Wanigeria now hawapo juu yetu, muziki wetu upo juu sasa.” – Diamond Platnumz.

No comments:

Powered by Blogger.