Wimbo wa 'Show Me' wa Harmonize na Rich Mavoko Wadaiwa Kuibwa...Mwenyewe Ajitokeza na Kudai Kuwa Ray C ni Shahidi..!!
‘Show Me’ ya Harmonize na Rich Mavoko ni moja kati ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, katika kipindi kifupi tangu itoke.
Imedaiwa kuwa, wimbo huo umeibiwa kutoka kwa msanii wa Bongo ambaye anaishi Uingereza ajulikanaye kama PCK. Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, msanii huyo amethibitisha kuibiwa wimbo wake huo, huku akimtaja Ray C kuwa ndio shahidi ambaye alikuwepo siku anairekodi.
“Kabla sijasafiri kuja UK nilienda WCB nikaonana na Laizer, walinicharge hela ya kurekodi pale, shilingi laki tano na nililipa ile pesa tukarekodi. Siku ambayo nilikuwa narekodi Ray C alikuwepo, nilipomaliza nikapewa tarehe ya kuja kuchukuwa nyimbo lakini siku ilipofika nikaanza kupigwa kalenda. Baadae nikaja kuambiwa imecollapse kwahiyo natakiwa kurekodi upya,” amesema msanii huyo.
“Kwenye process ya kurekodi upya nikawa napigwa chenga chenga. Nikawa nimesafiri, ilipofika majuzi
kati hapo Ray C aliniambia hebu ingia Instagram ya Harmonize kuna nyimbo ameipost lakini nikisikia beat
na melody ni kama ile nyimbo uliyokuwa unarekodi siku ile tulipokuwa studio,” ameongeza.
PCK amesisitiza kwa kusema, “Cha kunishangaza hakubadilisha neno hata moja. Beat ni ile ile na maneno ni, yale yale. Kinachoniuma, nashangaa mtu akilalamika mtu kaibiwa nyimbo yake, kisa tu ni mtu wa WCB kaifanya, unaambiwa unatafuta kiki, hapana. Siwezi kutafuta kiki kwa mtoto mdogo kama Harmonize, ambaye nina uwezo wa kumlisha miaka nenda rudi nikamuhudumia kila kitu. Nina mawakili wangu ambaowapo Tanzaniawanalifuatilia na
ninafikiri next week hilo swala litafikishwa mahakamani.”

No comments: